• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Maambukizi ya virusi vya korona hayatabadili maendeleo ya muda mrefu ya biashara ya China na nje

  (GMT+08:00) 2020-02-24 17:18:30

  Wizara ya Biashara ya China imesema maambukizi ya virusi vya korona COVIC-19 hayatabadili mwelekeo wa maendeleo ya muda mrefu ya biashara ya China na nchi za nje na nguvu ya ushindani ya China katika kuvutia fedha za kigeni, na China itaendelea kuwa sehemu inayowekezwa zaidi na kampuni za kimataifa.

  Akizungumza na waandishi wa habari hii leo, msaidizi wa waziri wa biashara wa China Ren Hongwu amesema, tangu kulipuka kwa maambukizi ya virusi vya korona, Wizara hiyo imetoa sera 20 zinazolenga "kutuliza biashara ya kigeni, kutuliza uwekezaji wa kigeni na kuhimiza matumizi" ili kusaidia kampuni zinazofanya biashara na nje kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo ugumu wa kupokea oda, ugumu wa kutekeleza mikataba, tatizo la usafirishaji bidhaa kimataifa na vikwazo vya kibiashara, na idara za mambo ya fedha, Benki Kuu ya China na idara ya forodha pia zimetoa sera za kuziunga mkono kampuni hizo. Vilevile, serikali za mitaa pia zimechukua hatua za kuzisaidia kampuni hizo kupita wakati huu wa taabu.

  "Hivi sasa, Guangdong, Jiangsu, Beijing, Shanghai na Sichuan zimeanza tena uzalishaji kwa haraka, na mkoani Zhejiang, kampuni zinazozalisha bidhaa zenye thamani ya zaidi ya dola za kimarekani milioni 10 zimeanza uzalishaji."

  Ren Hongwu amesema Wizara ya Biashara ya China itachukua hatua zaidi ikiwemo kuboresha mpangilio wa masoko ya kimataifa, kuzisaidia kampuni hizo kwa usahihi, na kuunga mkono biashara ya kuvuka mipaka kwenye mtandao wa internet ili kutuliza hali ya biashara ya kigeni ya China wakati inapofanya vizuri kazi ya kukinga na kudhibiti maambukizi ya virusi.

  "Kwa mujibu wa hali ya sasa, athari mbaya inayoletwa na maambukizi ya virusi vya korona kwa biashara ya kigeni ni ya muda, na biashara ya China na nje ina uwezo mkubwa wa kuhimili changamoto, na ina nguvu kubwa ya ushindani, haswa kwa kuwa kampuni hizo zina uwezo katika kufanya ubunifu na kupanua masoko, hivyo biashara ya kigeni ya China itaendelea kuongezeka kwa muda mrefu."

  Katika kutuliza fedha za kigeni, Ren Hongwu amesema tangu kutokea kwa maambukizi ya virusi vya korona, vizuizi vya usafirishaji wa watu na bidhaa na ukosefu wa uhakika wa malighafi vimeziletea kampuni hizo changamoto katika uzalishaji.

  "Inakadiriwa kuwa athari inayoletwa na maambukizi ya virusi kwa uvutiaji wa fedha za kigeni itakuwa kubwa katika robo ya kwanza ya mwaka huu, lakini athari hii ni ya muda na inaweza kudhibitiwa. Kwa muda mrefu, nguvu ya ushindani ya China katika kuvutia fedha za kigeni haijabadilika, na kampuni nyingi za kimataifa zina imani na hazijabadilisha mikakati yao kuhusu kuwekeza China, na kwamba China bado ni chaguo zuri kwa uwekezaji wa kimataifa."

  Ren Hongwu amesema, katika siku za baadaye, Wizara ya Biashara ya China itahimiza kampuni zaidi zinazofanya baishara na nchi za nje kuanza tena uzalishaji, kufuatilia vizuri utekelezaji wa miradi mikubwa inayowekezwa na fedha za kigeni, kuendelea kupanua maeneo yanayoruhusiwa kuwekezwa na nchi za nje, kuboresha maeneo maalumu ya kiuchumi, na kulinda vizuri maslahi halali na kuboresha mazingira ya uwekezaji kwa kampouni za nje.

  Habari nyingine zinasema, kuhusu athari iliyoletwa na COVID-19 kwa uchumi wa dunia, Shirika Kuu la Utangazaji la China limetoa tahariri ikisema, juhudi za China kukabiliana na maambukizi ya virusi na kurejesha uzalishaji wa kawaida si kama tu ni kwa ajili ya maslahi ya Wachina, bali pia ni kwa ajili ya dunia nzima.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako