• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China haitakaa kimya ikipakwa matope

    (GMT+08:00) 2020-02-24 19:58:46

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Zhao Lijian amesema, China haitakuwa "kondoo anayekaa kimya" pale inapotolewa maneno ya kashfa.

    Kauli hiyo imekuja baada ya wafanyakazi 53 wa Gazeti la Wall Street Journal la Marekani wanaofanya kazi nchini China alhamis iliyopita kuandika barua pepe kwa wakuu wa gazeti hilo, na kuwataka kuomba radhi kwa kutoa makala inayoitukana China. Lakini jumamosi iliyopita, msemaji wa gazeti hilo alisisitiza kuwa msimamo wa gazeti hilo bado haujabadilika.

    Zhao amesema uhuru wa utoaji wa tahariri si sababu ya gazeti hilo kupaka matope China, endapo gazeti hilo likiendelea kukataa kuomba radhi, litawajibika na matokeo yote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako