• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bunge la China lapitisha uamuzi wa kuzuia biashara haramu na ulaji wa wanyamapori

    (GMT+08:00) 2020-02-24 20:07:36

    Kamati Kuu ya Bunge la Umma la China limepitisha uamuzi wa kuzuia kikamilifu biashara haramu ya wanyamapori na kukataza ulaji wa wanyama pori ili kulinda maisha na afya ya wananchi wake.

    Pamoja na mambo mengine, hatua hiyo inalenga kulinda usalama wa kibaiolojia na ikolojia na kuzuia kikamilifu hatari kubwa kwa maisha ya watu. Uamuzi huo unaelekeza kuwa matumizi haramu na biashara ya wanyamapori inapaswa kupewa adhabu kali.

    Habari nyingine zinasema, Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC) limeshauriwa na Kamati ya Mwenyekiti kuahirisha mkutano wake wa mwaka.

    Mkutano wa tatu wa Kamati Kuu ya 13 ya CPPCC ulipangwa kuanza tarehe 3 mwezi ujao hapa Beijing.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako