• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakulima Tanzania watakiwa kuchangamkia fursa zao rozela

    (GMT+08:00) 2020-02-24 20:11:08

    Wakulima nchini Tanzania wametakiwa kuchangamkia fursa ya zao la rozela katika masoko, wakitakiwa kulima kwa wingi kutumia njia ya kilimo hai.

    Wito huo ulitolewa na Mkurugenzi wa Shirika la Kilimo endelevu Tanzania (SAT), Janeth Maro, kwenye ziara ya waandishi wa habari wa kilimo hai kwenye Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Hai inayomilikiwa na shirika hilo wilayani Mvomero, mkoani Morogoro.

    Maro alisema rozela ni moja ya zao lenye soko kubwa ndani na nje ya nchi lakini wakulima wengi bado hawajui fursa zilizopo kwenye zao hilo.

    Alisema rozela ya Tanzania ina soko kubwa nje ya nchi hasa kwenye nchi ya Uswisi na kwamba taasisi hiyo imekuwa ikipeleka zao hilo wanalolima kwenye kituo chao kwa njia ya asili.

    Alisema mazao mengine yenye soko nchini Uswisi ni pamoja na mazao ya viungo, mdarasini na pilipili manga, pia wapo kwenye hatua ya mwisho kupeleka nchini humo tani 10 mpaka 15.

    Alisema zao hilo halina ugumu kwenye kulima kwa kuwa linapaliliwa, linaota na kustawi kwenye mvua chache hasa ikinyesha wakati wa kukaribia mavuno.

    Alisema kwa Tanzania zao hilo linastawi zaidi kwenye maeneo ya Mvomero ambako kuna mvua ndogo kwa mwaka na maeneo mengine yenye hali kama ya wilaya hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako