• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wataalamu wa WHO wasema hatua za China za kupambana na COVID-19 zimepata mafanikio

  (GMT+08:00) 2020-02-25 09:07:15

  Baada ya kufanya ukaguzi nchini China kwa siku 9, jopo la wataalamu wa China na shirika la afya duniani WHO, jana lilifanya mkutano na waandishi wa habari hapa Beijing. Kiongozi wa watalaamu wa nchi za nje ambaye pia ni mshauri mwandamizi wa katibu mkuu wa WHO Bw. Bruce Aylward amesema,

  "baada ya kufanya ukaguzi kwa makini na kwa pande mbalimbali, watalaamu wanaona hatua zilizochukuliwa na China kupambana na virusi hiyo, zimezuia kwa ufanisi hali ya kuenea kwa virusi hivyo kwa kasi. Wiki mbili zilizopita nilipofika China, kila siku wagonjwa wapya zaidi 2,000 waliripotiwa, wakati tulipomaliza kazi yetu, idadi ya wagonjwa waliothibitishwa jana ilikuwa 416, ambayo imepungua kwa asilimia 80 ndani ya wiki mbili, na takwimu hiyo ni sahihi. "

  Bw. Bruce Aylward pia amesema tathmini ya kundi hilo imeona kuwa, hatua zinazochukuliwa na China kuhamasisha serikali na watu wote katika jamii kupambana na maambukizi ya virusi hiyo, zimegeuza hali ya kupamba moto kwa maambukizi hayo, kuzuia maelfu ya wagonjwa wapya kutokea, na hayo ni mafanikio makubwa.

  Kundi hilo pia limependekeza nchi mbalimbali kufanya kazi ya usimamizi na ukaguzi, ili kuwagundua mapema, kuwathibitisha mapema, kuwaweka karantini mapema na kuwatibu mapema wagonjwa wa virusi hivyo, na pia kuwafuatilia na kuwaweka karantini watu waliokaribiana na wagonjwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako