• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Idadi ya vifo kutokana na virusi vya korona nchini Italia yafikia saba

  (GMT+08:00) 2020-02-25 09:11:15

  Idadi ya vifo kutokana na virusi vya korona nchini Italia imeongezeka na kufikia 7 baada ya mkoa wa kaskazini wa Lombardy kutangaza kifo cha mwanaume mwenye umri wa miaka 62 jana usiku.

  Miji kumi ya mkoa huo imewekewa vizuizi ambako mgonjwa wa kwanza wa virusi hivyo alitambuliwa tarehe 21 mwezi huu.

  Timu ya wataalam wa Shirika la Afya Duniani WHO na taasisi ya kuzuia na kudhibiti ugonjwa ya Ulaya ECDE, imewasili nchini Italia ili kuzisaidia mamlaka nchini humo kufahamu zaidi hali ya maambukizi ya virusi hivyo vya COVID-19.

  Habari pia zinasema wizara ya afya ya Ujerumani imerekebisha tathmini yake kuhusu hali ya mlipuko wa virusi hivyo, na kusema virusi hivyo vina hatari ya kuenea nchini humo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako