• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Zaidi ya wajumbe 6,000 wanatarajiwa Uganda katika kongamano la tatu la G77

    (GMT+08:00) 2020-02-25 18:05:09

    Mkutano wa kilele wa tatu wa G77 wa Umoja wa Mataifa, utaandaliwa jijini Kampala mwezi wa nne mwaka huu, kuanzia tarehe 17-19.

    Mkutano huo, utahudhuriwa na zaidi ya wajumbe 6000 kutoka mataifa 135. Lengo kuu la G77 ni kukuza malengo ya kustawisha uchumi wa mataifa wanachama , hali kadhalika kuboresha mazingira ya kufanyia biashara.

    Mkutano wa kilele wa G77 huleta pamoja mataifa yenye uchumi mdogo, yale ya uchumi ibuka na wastani kujadiliana maswala mbali mbali ya kibiashara ili kusaidiana kimaendeleo.

    Marais na wajumbe wao, wanatarajiwa jijini Kampala kwenye mkutano huo, na hii itakuwa fursa ya kipekee kwa Uganda kujitangaza kote duniani.

    Ajenda kuu za mkutano huo ni maswala ya kukuza biashara kati ya mataifa wananchama, uwekezaji, misaada kwa mataifa wanachama na maswala mengine ya kijamii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako