• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ujerumani kuisaidia Kenya 'Mabilioni' ya fedha kwaajili ya miradi hii

    (GMT+08:00) 2020-02-25 18:06:12

    Serikali ya Ujerumani imeahidi kufadhili miradi ya elimu, na uzalishaji wa viwanda nchini Kenya ili kukabiliana na tatizo la ajira ambalo linazidi kuongezeka nchini Kenya.

    Hayo yameelezwa leo baada ya rais uhuru Kenyatta wa Kenya na mwezake wa Ujerumani Frank-Walter Steimeier kutia sahihi mikataba ya ushirikiano wa kibiashara na maendeleo baina ya mataifa hayo mawili jijini Nairobi, Kenya.

    Kwenye mkutano wao ulioandaliwa katika ikulu ya Nairobi, rais Kenyatta aliipongeza serikali ya Ujerumani kwa kujitolea kwake kufadhili miradi ya elimu nchini Kenya, kuanzia shule za msingi hadi kwenye taasisi za masomo ya juu na kukiri kuwa hatua hiyo itasaidika pakubwa katika kuboresha uchumi na maisha ya wakenya.

    Serikali ya Ujerumani imekubali kushirikiana na Kenya katika sekta za uzalishaji na kilimo kwa kufadhili viwanda vya uzalishaji sawa na kuwaleta wataalam wa viwanda na biashara kusaidia wastawishaji nchini Kenya. Steinmeier aliafiki kuwa taifa lake lina mengi ya kujifunza ili kuweza kuwekeza katika maeneo ambayo ni ya msingi. Rais Steinmeier amefuatana na ujumbe wa wafanyibiashara kutoka Ujerumani wanaolenga kuwekeza katika sekta mbali mbali ya uchumi wa nchi ya Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako