• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Reli ya SGR nchini Kenya yaendeshwa kwa usalama kwa siku elfu moja

  (GMT+08:00) 2020-02-26 09:18:13

  Meneja mkuu wa uendeshaji wa reli ya SGR wa kampuni ya Afistar Bw. Li Jiuping, amesema reli ya SGR ya Kenya imeleta manufaa kwa jamii na uchumi wa Kenya.

  Kwenye sherehe ya kufikisha siku ya elfu moja ya uendeshaji salama wa reli ya SGR iliyofanyika mjini Nairobi, Bw. LI amesema tangu reli hiyo ianze kazi tarehe 31 Mei, mwaka 2017, hakuna ajali yoyote iliyotokea na kufungua ukurasa mpya katika historia ya reli nchini Kenya.

  Bw. Li pia amesema hivi sasa asilimia 80 ya wafanyakazi wa reli hiyo ni wenyeji. Kampuni yake imetoa mafunzo kwa wakenya na kulenga kuwapatia teknolojia ya reli ya China, ili kusaidia Kenya kuwa na akiba ya nguvukazi katika sekta ya reli.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako