• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Idadi ya watu walioambukizwa COVID-19 nchini Italia yaongezeka na kufikia 322

  (GMT+08:00) 2020-02-26 09:35:44

  Kamishna maalumu wa matukio ya dharura na mkuu wa idara ya ulinzi wa umma ya Italia Bw. Angelo Borrelli, ametangaza kuwa watu 322 wamethibitishwa kuambukizwa COVID-19 nchini humo, na 10 kati yao wamefariki dunia.

  Ameongeza kuwa serikali ya Italia imefunga wilaya 11, ambazo 10 kati yake ziko katika mkoa wa Lombardy, na wilaya moja iko katika eneo la Veneto mjini Venice.

  Mbali na hayo, wizara ya afya ya Ufaransa jana imetangaza kuwa watu wawili wamethibitishwa kuambukizwa COVID-19, na kuifanya idadi ya maambukizi iongezeke na kufikia 14 nchini humo. Serikali ya Ufaransa imesema mpaka kati ya Ufaransa na Italia hautafungwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako