• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kanda 26 za ngazi ya mkoa nchini China zatoa ripoti kuwa hakuna mgonjwa mpya wa COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-02-27 10:12:43

    Kanda 26 kati ya kanda 31 za ngazi ya mkoa katika China bara zimetoa ripoti kwamba hakuna mgonjwa mpya wa COVID-19.

    Kamisheni ya afya ya taifa ya China NHC na idara za afya za mikoa zimetoa takwimu mpya zikionesha kuwa China bara imeripoti jumla ya wagonjwa 406 wapya wa COVID-19, ambao ni pamoja na wagonjwa 401 mkoani Hubei, mmoja huko Shandong, Shanghai na Hebei, na wawili mkoani Sichuan.

    Aidha, idadi ya wagonjwa wapya nje ya mkoa wa Hubei ambao ni kiini cha mlipuko wa COVID-19, imeshuka na kufikia 9 ya jumatatu kutoka 11 ya jumapili iliyopita.

    Msemaji wa kamisheni hiyo Bw. Mi Feng amesema, China bara, mbali na mkoa wa Hubei, jumanne haikuwa na ripoti yoyote kuhusu vifo vipya vilivyotokana na COVID-19 na idadi ya wagonjwa mahututi imepungua kwa 25.

    Ameongeza kuwa kutokana na kuongezeka kwa madaktari na njia za matibabu zinazoboreshwa, idadi ya wagonjwa wa COVID-19 waliotibiwa na kutoka hospitali inaendelea kuongezeka kote nchini China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako