• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ni asilimia 3.5% ya wanyarwanda walioomba mikopo benki mwaka 2019

    (GMT+08:00) 2020-02-27 18:34:50

    Idadi ya wanyarwanda wanaoomba mikopo kutoka benki za kibiashara inaendelea kuongezeka lakini takwimu zinasalia kuwa chini,huku takwimu rasmi zikionyesha kuwa ni watu 421,000 tu ambao walichukua mikopo mwaka uliopita.

    Hii inawakilisha asilimia 3.5 ya idadi ya watu.

    Kuweka hii katika muktadha ,idadi hii ni ndogo kuliko idadi ya watu katika wilaya ya gasabo,ambayo ina watu takriban 500,000.

    Rwanda ina wilaya 30.

    Takwimu zilizotolewa na Benki Kuu ya Rwanda zinaonyesha kuwa ni watu wachache waliiomba mikopo mwaka 2018 (308,000) .

    Mikopo iliyotolewa na benki za kibiashara kufikia mwishoni mwa mwaka 2019 ilikuwa Rwf2,084 bilioni,lakini takwimu hizo zinasema kuwa mikopo hiyo ni pamoja na ile ile iliyopewa mashirika mbalimbali.

    Kulingana na utafiti wa Rwanda FinScope uliotolewa mwaka 2017,ni asilimia 26 tu ya wanyarwanda ambao wana akaunti rasmi za benki.Hata hivyo utafiti huo uliweka ujumuishwaji wa kifedha katika silimia 89.Hii inamaanisha kuwa raia walipata huduma za fedha kupitia majukwaa mengine,badili ya benki za kibiashara.

    Wadadisi wa masuala ya uchumi wanasema,hii inaweza kwa kiwango fulani,kufafanua ni kwa nini benki nyingi nchini humo zinalenga katika kutoa huduma kwa mashirika na sio watu binafsi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako