• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa wito wa uratibu wa pamoja na Japan na Korea Kusini dhidi ya kuenea kwa maambukizi ya COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-02-27 18:56:41
    Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi kwa nyakati tofauti amezungumza kwa simu na wenzake wa nchi jirani za Japan na Korea Kusini, ambazo hivi karibuni zimeshuhudia kuongezeka kwa wagonjwa walioambukizwa virusi vya korona.

    Katika mazungumzo hayo, Wang Yi alisema China na Japan zinapaswa kuongeza uratibu ili kuzuia kuenea kwa virusi vya korona (COVID-19), na nchi hizo mbili kuendelea na ushirikiano wa kichumi na kibiashara kama kawaida kunachangia utulivu wa uchumi duniani. Alisisitiza kuwa, China inafuatilia hali ya maambukizi nchini Japan, na imetoa msaada wa vifaa vya kinga kutokana na matakwa ya Japan. Pia China iko tayari kutoa msaada wa kulingana na uwezo wake, endapo Japan itatoa maombi.

    Akizungumza na mwenzake wa Korea Kusini, Wang Yi alisema uzoefu uliopatikana na China unaonyesha kuwa, kuchukua hatua mapema na kupunguza safari za watu ni muhimu sana katika kuzuia kuenea kwa virusi, na China inapenda kubadilishana uzoefu na Korea Kusini, na kutoa msaada unaohitajika ili kuunga mkono serikali ya Korea Kusini na watu wake katika vita dhidi ya virusi vya korona.

    Habari nyingine zinasema, mjumbe wa ofisi ya siasa ya kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC Yang Jiechi ambaye pia ni mkurugenzi wa ofisi ya Tume ya Masuala ya Kigeni ya Kamati hiyo, atafanya ziara kesho na kesho kutwa nchini Japan, na kufanya mazungumzo ya raundi mpya ya siasa ya ngazi ya juu kati ya China na Japan. Akizungumzia hilo, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Zhao Lijian amesema ziara ya Yang Jiechi wakati huu imeonesha kuwa China inazingatia sana uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako