• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Pato la Taifa la Zanzibar latarajiwa kukua kwa asilimia 7.3 mwaka 2020

    (GMT+08:00) 2020-02-27 21:12:34
    Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema Pato la Taifa la mwaka 2020 linatarajiwa kukua kwa kasi ya wastani wa asilimia 7.3 kutoka asilimia 7.0 ya mwaka 2019.

    Akiwasilisha hotuba ya mwelekeo wa hali ya uchumi ,mpango wa maendeleo na bajeti kwa mwaka 2020/21 -2022/23 jana, katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi , Waziri wa Fedha na Mipango Balozi Mohammed Ramia alisema ongezeko hilo linatokana na matarajio ya kuongezeka kwa wawekezaji wa miradi ya maendeleo .

    Balozi Ramia alisema mapato ya ndani kwa kipindi cha miaka mitatu yanakadiriwa kufikia asilimia 26.0 ya Pato la Taifa kwa miaka 2019 -2022 kutoka wastani wa asilimia 24.2 ya mwaka 2018/19.

    Wakichangia hotuba hiyo,wajumbe wa Baraza la Wawakilishi waliishauri serikali kuweka kipaumbele katika miradi ya maendeleo itakayosaidia kuongeza uchumi na Pato la Taifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako