• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kilavuka achaguliwa Afisa Mtendaji Mkuu mpya wa Kenya Airways

    (GMT+08:00) 2020-02-28 18:59:47
    Halmashauri ya shirika la ndege la Kenya, Kenya Airways imemuidhinisha Allan Kilavuka kuwa Afisa Mtendaji Mkuu mpya wa shirika hilo kuanzia Aprili 1, 2020.

    Hadi kuchaguliwa kwake, Kilavuka alikuwa akikaimu nafasi hiyo tangu Disemba 16, kufuatia kuondoka kwa Sebastian Mikos.

    Pia alikuwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Jambojet linalomilikiwa na Kenya Airways.

    Tayari, Kenya Airways inatarajiwa kutangaza hasara ya shilinhgibilioni Ksh.9.5 na shirka hilo limekuwa likishindwa kupata ufanisi katika oparesheni zake.

    Kilavuka ana uzoefu wa zaidi ya miaka 23 katika uongozi baada ya kufanya kazi katika sekta mbali mbali ikiwa ni pamoja na mikakati na kifedha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako