• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Naivas yazindua mpango wa kuuza bidhaa kwa mkopo

    (GMT+08:00) 2020-02-28 19:00:08
    Maduka makubwa ya Naivas nchini Kenyakwa kushirikiana na kampuni ya Aspira imezindua mpango wa kuuza bidhaa kwa mkopo kwa wateja wake.

    Chini ya mpango huo Naivas itawawezesha wateja wake kupata bidhaa za matumizi ya nyumbani na kulipia kwa malipo kwa kipindi cha mwaka mmoja kwa awamu za kila siku au ya kila mwezi.

    Akiongea wakati wa uzinduzi rasmi wa mpango wa kwa jina Lipabaadaye katika tawi la Naivas la Gateway, Afisa Mkuu wa Biashara Willy Kimani alisema kuwa mpango huo unawezeshwa kupitia ushirikiano wake na Aspira, ambao hufanya ufadhili wa mikopo.

    Alisema utafiti wa pamoja na Aspira, ulionyesha kuwa Wakenya wanapendelea kumiliki bidhaa za ubowa wa juu za nyumbani, pamoja na vifaa vya elektroniki na samani na wanahitaji huduma itakayowawezesha kulipa pole pole.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako