• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaongeza kwa wingi wa mabilionea

    (GMT+08:00) 2020-02-28 19:01:02
    China , Marekani na India zimechukua nafasi tatu za juu kwa kuwa na idadi kubwa zaidi ya mabilionea.

    Takwimu kutoka kwa Orodha ya matajiri wa Dunia ya Hurun 2020, inasema China kwa sasa ina mabilionea 799, ambao ni wengi zaidi ulimwenguni. Mwaka huu wa 2020 kumekuwa na mabilionea 182 waliojiunga kwenye orodha ya dunia.

    Marekani iko kwenye nafasi ya pili na mabilionea 626 , India, Ujerumani na Uingereza zote zina zaidi ya mabilionea 100.

    Mtu tajiri zaidi duniani kulingana na orodha hiyo ni Jeff Bezos, ambaye ni mwanzilishi wa biashara ya mtandaoni ya Amazon, akiwa na dola bilioni 140.

    Mkurungezi wa LVMH Bernard Arnault yuko kwenye nafasi ya pili naye mwanzilishi wa Microsoft Bill Gates akiwa nafasi ya 3.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako