• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasema hatua zake za kuzuia COVID-19 zinalenga wote wanaotoka sehemu zinazoathiriwa na virusi

    (GMT+08:00) 2020-02-28 19:57:41

    Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Zhao Lijian leo hapa Beijing amesema, hatua za kukabiliana na maambukizi ya virusi vipya vya korona COVID-19 zinazochukuliwa na China zinawalenga watu wote, wachina ama wageni wanaotokea sehemu zinazoathiriwa vibaya na virusi hivyo.

    Zhao amesema, hivi sasa China iko katika kipindi kigumu katika kuzuia na kudhibiti virusi vya korona, na sehemu mbalimbali zimechukua hatua kali kuzuia maambukizi mapya yasitokee. Baada ya kesi nyingi kuripotiwa nje ya China, Beijing imeimarisha usimamizi wa afya kwa watu wanaoingia mjini humo, na wale wanatoka sehemu zenye hali mbaya ya maambukizi wanatakiwa kukaa nyumbani kwa siku 14 ili kuangalia afya zao. Zhao amesisitiza kuwa, hatua za karantini zinazochukuliwa na China zimetambuliwa na wataalam wa Shirika la Afya Duniani kuwa sahihi, na zimeonesha ufanisi wake katika kupunguza kasi ya maambukizi na kuzuia maambukizi ya virusi kati ya watu.

    Wakati huohuo, Zhao amesema China inashukuru Umoja wa Ulaya kwa kutambua juhudi zake katika kupambana na COVID-19, na kusema China inapenda kushirikiana na pande mbalimbali kukabiliana na changamoto za afya ya umma za sasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako