• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Manchester City yashinda taji la tatu mfululizo la Carabao, Mtanzania Samatta aipachikia Villa bao la kichwa

    (GMT+08:00) 2020-03-02 10:04:45

    Aston Villa timu anayokipiga Mbwana Samatta, jana Machi Mosi ilishuhudia ubingwa ukiponyoka na kuangukia mikononi mwa wapinzani wao Manchester City. Villa iliyo chini ya Dean Smith ilikubali kichapo cha mabao 2-1 kwenye mchezo wa fainali wa Kombe la Carabao uliyochezwa Uwanja wa Wembley. City ilianza kuandika bao la kwanza dakika ya 20 kupitia kwa Muargentina Sergio Arguero akimalizia pasi ya Philip Foden na bao la pili dakika ya 30 kupitia kwa Rodri Hernandez akimalizia pasi ya İlkay Gundogan. Samatta alipachika bao dakika ya 41 kwa kichwa kilichozama nyavuni jumlajumla akimalizia pasi ya kiungo Mholanzi, Anwar El Ghazi. Baada ya kazi yake nzuri ambayo hata hivyo haikuisaidia Aston Villa kupata taji, kocha Dean Smith alimpumzisha Samatta dakika ya 80 na kumuingiza kinda wa England, Keinan Davis.

    Ushindi huo unamaanisha Manchester City inatwaa taji la Carabao kwa mara ya tatu mfululizo na kujifariji katika msimu ambao hawana matokeo mazuri kwenye Ligi Kuu. Timu ya mwisho kucheza na City fainali ilikuwa ni Watford na ilichapwa mabao 6-0 na ilipocheza na Arsenal 2015 aliichapa 4-0 hivyo Samatta amefanya maajabu maana wengi walidhani ingechapwa mabao saba.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako