• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mtaalamu wa China apendekeza kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika mapambano dhidi ya janga la nzige

    (GMT+08:00) 2020-03-02 17:38:36

    Hivi karibuni jamii ya kimataifa imefuatilia kwa karibu janga la nzige katika Afrika, Asia ya Magharibi na Asia ya Kusini. Mtaalamu wa China Bw. Zhang Zehua anaona kuwa inapaswa kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika mapambano dhidi ya janga hilo.

    Katika miezi kadhaa iliyopita, nchi nyingi zimekabiliwa na janga la nzige. Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa (FAO), janga hilo limeathiri nchi zaidi 20. Wachambuzi wanasema, kama hatua zozote za udhibiti hazitachukuliwa, idadi ya nzige huenda itaongezeka kwa mara 500 ifikapo mwezi Juni mwaka huu, na huenda wataenea katika nchi 30 za Afrika na Asia.

    Kwa nini janga hilo la nzige ni mbaya namna hii? Mtafiti wa taasisi ya utafiti wa uhifadhi wa mimea katika Chuo cha Sayansi ya Kilimo cha China Bw. Zhang Zehua amesema, janga hilo linahusiana na mvua za kutosha katika maeneo hayo kutoka mwaka 2018 hadi mwaka 2019.

    "Mvua za kutosha zimetoa mazingira mazuri kwa nzige wa jangwa kuzaliana na kuongezeka, hivyo katika mwaka 2019, idadi ya nzige imeongezeka kwa kiwango kikubwa. Kuanzia mwanzoni mwa mwaka huu, nzige wadogo wametoka kwenye ardhini, na wana chakula cha kutosha, mazingira mazuri, na hali nzuri ya unyevu. Kasi ya uhamaji wa nzige ni kubwa, hivyo maafa ya nzige yaongezeka kwa kasi. "

    Bw. Zhang Zehua anaona kuwa, janga la nzige siyo suala la sehemu zinazoathiriwa tu, pia ni suala la kimataifa, na ni muhimu hatua za tahadhari na kukabiliana janga la nzige zichukuliwe, sambamba na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa.

    "Hili ni janga linaloathiri dunia nzima, kuna hasara za moja kwa moja, pia kuna hasara za maeneo na za kiundani, huenda zitafanyiwa tathmini baada ya miaka kadhaa. Inahitaji kujenga utaratibu wa mawasiliano ya ushirikiano wa kimataifa, na jumuiya ya kimataifa kukabiliana nayo kwa pamoja. Vilevile, tunaweza kupitia ushirikiano huo wa kimataifa, kutoa uzoefu na ustadi wetu wa kinga na udhibiti wa janga la nzige kwa nchi nyingine. "

    Habari zinasema, katika miaka ya hivi karibuni, uwezo wa China katika usimamizi, utoaji tahadhari, kinga na udhibiti wa nzige umeongezeka, teknolojia za kinga na udhibiti ziko katika kiwango cha juu duniani, na akiba ya dawa na vifaa vya udhibiti wa nzige pia ni kutosha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako