• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afrika Mashariki

    (GMT+08:00) 2020-03-02 18:44:16

    Wanaafrika Mashariki watalazimika kununua nguo za mitumba kwa bei ghali mno endapo serikali za mataifa husika zitaongeza ushuru kwa nguo zinazonunuliwa kutoka mataifa ya nje ya ukanda wa Afrika Mashariki.

    Ripoti zinasema kwamba huenda ushuru wa kati ya asilimia 30 hadi 35 ukaongezwa kwa nguo za mitumba kutoka nje ya Afrika Mashariki. Hii ni mojawapo ya hatua za kulinda viwanda vya nguo vilivyopo katika ukanda huu.

    Kando na mitumba, ushuru mwingine utakaongezwa bi ule wa vyuma, mbao na bidhaa zake kutoka nje ya ukanda wa Afrika Mashariki. Sekta za kibinafsi za biashara zinapendekeza ushuru wa asilimia 32.5 kwa bidhaa zote kutoka nje ya Afrika Mashariki, ili kulinda biashara za ndani kwa ndani.

    Pendekezo hili litawasilishwa kwenye kongamano la Jumuiya ya Afrika Mashariki itayawaleta pamoja marais wote wa mataifa husika, jijini Arusha Tanzania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako