• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ulinzi wa hakimiliki za ubunifu nchini China wachochea ukuaji wa maombi ya hakimiliki za kigeni

    (GMT+08:00) 2020-03-02 19:15:08

    Japan, Marekani na Ujerumani zimeongoza kwenye orodha ya maombi ya hakimiliki nchini China kwa mwaka jana.

    Kamati ya Taifa ya Hakimiliki za Ubunifu ya China imesema, masoko kutoka nchi na sehemu 186 ziliomba hataza na chapa nchini China mwaka 2019, ikiwa ni ongezeko la asilimia 12 dhidi ya ile ya mwaka 2018, huku Japan, Marekani, na Ujerumani ziliomba hataza nyingi zaidi za uvumbuzi.

    Kamati hiyo imesema maendeleo hayo yametokana na sheria kali na kukabiliana kikamilifu na mapungufu katika utoaji wa haki miliki. Kuanzia mwaka 2019, China ilitunga mfululizo wa sheria, kanuni na mwongozo wa ulinzi wa hakimiliki za ubunifu, ikiwemo Sheria ya Uwekezaji ya Kigeni, ili kuanzisha mazingira ya usawa, uwazi na yanayotabirika kwa wawekezaji wa kigeni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako