• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yawataka wananchi wake kutowatendea vibaya raia wa kigeni kutokana na mlipuko wa COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-02 19:47:16

    Serikali ya Kenya imewataka wananchi wake kutowatendea vibaya raia wa kigeni walioko nchini humo kutokana na tishio la mlipuko wa ugonjwa wa nimonia inayosababishwa na virusi vipya vya korona (COVID-19).

    Akizungumza na waandishi wa habari jijini Nairobi mara baada ya mkutano wa kwanza wa Kamati ya Dharura ya Taifa kuhusu Virusi vya Korona, waziri wa afya nchini Kenya Mutahi Kagwe amesema kumekuwa na matukio ambapo wakazi wa maeneo husika wamewatendea vibaya wageni kutoka nchi za nje kutokana na ubaguzi.

    Amesema serikali imeimarisha ufuatiliaji wa virusi hivyo katika mipaka yote ya kuingia nchini humo, nje ya viwanja vya kimataifa vya ndege. Pia amesema, nchi hiyo utafanya uratibu na nchi jirani zake, hususan Jumuiya ya Afrika Mashariki, kuhusu hatua za kivitendo ili kukabiliana na tishio linalotokana na virusi vya korona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako