• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi za Afrika zajitahidi kupambana na COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-03 19:17:40

    Maambukizi ya ugonjwa wa nimonia inayosababishwa na virusi vipya vya korona COVID-19 yameanza kuenea katika nchi za Afrika, na jana, Senegal, Morocco na Tunisia kwa nyakati tofauti zimeripoti mgonjwa kwa kwanza wa COVID-19. Nchi za Afrika zinajiandaa kupambana na maambukizi hayo. 

    Jana, waziri wa afya na maendeleo ya jamii nchini Senegal Abdoulaye Diouf Sarr, amethibitisha kuwa, raia mmoja wa Ufaransa anayeishi nchini Senegal amethibitishwa kuambukizwa na COVID-19. Mtu huyu aliwasili Senegal kutokea Paris tarehe 26 mwezi uliopita. Rais Macky Sall wa Senegal amekubali kuteng dola za kimarekani milioni 2.4 kupambana na maambukizi ya virusi hiyo.

    Nchini Morocco, raia mmoja wa nchi hiyo anayeishi nchini Italia amethibitishwa kuambukizwa na virusi hivyo wakati aliporudi Morocco, huku waziri wa afya nchini Tunisia, Abdellatif Mekki akitangaza kuwa, raia mmoja wa nchi hiyo aliyerudi kutoka Italia tarehe 27 mwezi uliopita, amethibitishwa kuwa na maambukizi ya virusi hivyo.

    Ingawa nchi za Afrika Mashariki hazijaripoti mgonjwa wa virusi hivyo, lakini zimejiandaa kukabiliana na mlipuko huo endapo utatokea. Serikali ya Ethiopia imetangaza kuunda tume ya kitaifa ya mawaziri ambayo itasimamia kwa karibu juhudi za kudhibiti maambukizi ya COVID-19 nchini humo.

    Hatua hiyo imetolewa na Ethiopia, ambayo ni nchi ya pili yenye idadi kubwa ya watu barani Afrika, ikiwa na jumla ya watu milioni 107. Nchi hiyo pia imeongeza juhudi zake za kushirikiana na Shirika la Afya Duniani WHO kupambana na COVID-19, hasa kuongeza usimamizi na ufuatiliaji katika viwanja vya ndege vinne vya kimataifa na sehemu 21 za mipaka.

    Mkuu wa Kituo cha Dharura kilichoko kwenye Chuo cha Afya ya Umma nchini humo Zewdu Assefa amesema, Ethiopia inajenga kituo cha karatini, na kununua vifaa mbalimbali chini ya msaada wa WHO ili kuzuia na kudhibiti maambukizi hayo. Serikali ya nchi hiyo pia imetoa mafunzo kwa watu 60 watakaofuatilia virusi hivyo, kutoa huduma za matibabu kwa wagonjwa, kutoa elimu ya afya kwa umma, na kushughulikia taarifa zozote ambazo si za kweli kuhusiana na virusi hivyo.

    Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, (DRC) ilikabiliana na virusi vya Ebola. Mratibu wa mapambano dhidi ya Ebola nchini humo Jean-Jacques Muyembe amesema, uzoefu wa DRC wa kupambana na Ebola unaweza kusaidia kupambana na COVID-19. Amesema imechukua muda mrefu kutafiti dawa na chanjo ya Ebola, na uzoefu huo unasaidia kuharakisha kutafiti chanjo ya COVID-19.

    Amesema maambukizi ya COVID-19 na Ebola yanafanana, na hatua za kupambana na Ebola pia zinaweza kuchukuliwa katika mapambano dhidhi ya COVID-19, hasa kunawa mikono na kuvaa mask.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako