• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki ya Dunia yatangaza kutoa dola za kimarekani bilioni 12 kuzisaidia nchi zinazoathiriwa na COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-04 09:38:49

    Benki ya Dunia imetangaza kutoa dola za kimarekani bilioni 12 kuzisaidia nchi zinazoathiriwa na mlipuko wa nimonia ya COVID-19 inayosababishwa na virusi vipya vya korona.

    Msaada huo wa haraka utasaidia nchi zinazoendelea kuimarisha mifumo ya afya, ikiwemo kupanua upatikanaji wa huduma za afya ili kuwakinga watu dhidi ya ugonjwa huo, kuimarisha usimamizi wa ugonjwa, kuboresha mwitikio juu ya masuala ya afya ya umma, na kushirikiana na sekta binafsi katika kupunguza athari ya ugonjwa kwa uchumi.

    Msaada huo wa kifedha umekuja siku moja baada ya Shirika la Fedha la Kimataifa IMF na Benki ya Dunia kusema kwenye taarifa ya pamoja kuwa wako tayari kuzisaidia nchi wanachama kukabiliana na janga hilo na changamoto za kiuchumi zinazotokana na mlipuko wa COVID-19.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako