• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalam wa WHO waipongeza China kwa kutoa uzoefu wake wa kupambana na COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-04 09:51:07

    Wataalam wa Shirika la afya duniani (WHO) wameipongeza China kwa kuchangia uzoefu wake na nchi nyingine katika kukabiliana nimonia ya COVID-19 inayosababishwa na virusi vya korona.

    Mkuu wa Mipango ya Dharura ya Afya wa WHO Bibi. Maria van Kerkhove amesema katika taarifa ya kila siku kwamba, uzoefu wa China katika kupambana na COVID-19 unahitajika, akitaja msaada wa hivi karibuni wa China wa kutuma wataalam na vifaa vya matibabu kwa Iran, ambao ni mfano mzuri.

    Mkurugenzi mtendaji wa mipango ya dharura ya afya wa WHO Bw. Michael Ryan, amesema serikali ya Iran inatarajia timu ya wataalam wa China na timu ya WHO wakutane kama ilivyotokea nchini China kuchangia uzoefu, na kuchukua hatua pamoja dhidi ya mlipuko wa COVID-19 nchini Iran.

    Wakati huohuo, mkurugenzi mkuu wa Shirika la afya duniani Bw. Tedros Ghebreyesus amesema uhaba wa vifaa vya kujikinga duniani unazuia uwezo wa nchi nyingi kukabiliana na virusi vya korona, na kutoa wito serikali na kampuni zinazohusika kuchukua hatua za haraka ili kuongeza uzalishaji na ugavi wa vifaa hivyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako