• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uturiki yaeleza sababu za kufungua mpaka wake na kuwaruhusu wahamiaji kuingia Ulaya

    (GMT+08:00) 2020-03-04 17:42:08

    Uamuzi wa Uturuki uliotolewa wiki iliyopita na rais Tayyip Erdogan wa kufungua mpaka wa nchi yake kuwaruhusu wahamiaji kukusanyika katika mpaka wa Ugiriki umepokelewa vibaya na baadhi ya wanasiasa wa Umoja wa Ulaya. Balozi wa Umoja wa Ulaya ameeleza kukasirishwa na hatua hiyo, na kusema uamuzi huo una lengo la kusaliti Umoja huo.

    Hata hivyo, baadhi ya wanadiplomasia wanakiri kuwa, rais Erdogan anaushurutisha Umoja wa Ulaya kwa kuwa nchi wanachama wake haziwezi kukubaliana jinsi ya kushughulika na wakimbizi na kuepuka marudio ya mgogoro wa wahamiaji wa mwaka 2015/16. Baadhi yao wanaamini Umoja huo utatoa fedha zaidi kwa Uturuki ili iendelee kuzuia wahamiaji wanaoingia Ulaya.

    Sasa swali ni kwamba, kwa nini Uturuki imefungua mpaka wake? Uturuki ilifungua mlango wake kwa wahamiaji wiki iliyopita baada ya shambulizi baya dhidi ya askari wa Uturuki lililofanywa na jeshi la serikali ya Syria katika sehemu ya kaskazini ya nchi hiyo, ambapo karibu askari 34 wa Uturuki waliuawa katika shambulizi hilo la anga. Rais Erdogan alijibu shambulizi hilo kwa kuangusha ndege mbili za kivita za serikali ya Syria jumapili iliyopita na moja jumanne.

    Mapigano ya kijeshi katika mkoa wa Idlib nchini Syria yamezua hofu ya kurejea kwa mapigano makubwa na kuwafanya wahamiaji zaidi wa Syria kukimbilia kwenye mpaka wa nchi hiyo na Uturuki. Watu milioni moja wamekimbia makazi yao tangu Desemba mwaka jana kuelekea karibu na mpaka wa kusini wa Uturuki, na kusababisha kile kinachoitwa na Umoja wa Mataifa kuwa ni mgogoro mbaya zaidi wa binadamu katika miaka tisa ya vita.

    Ikiwa tayari na wakimbizi milioni 3.6 wa Syria, Uturuki imedhamiria kuzuia kuingia kwa wahamiaji zaidi kutoka Syria, na ijumaa iliyopita, nchi hiyo ilifungua mpaka wake wa magharibi na kuwaruhusu wakimbizi kuingia Ulaya. Wataalam wanachambua hilo kwa kusema, kwa kuruhusu wahamiaji kuingia Ulaya kwa wakati huu, Uturuki inataka kuvutia ufuatiliaji wa kimataifa kwa mgogoro unaoendelea Idlib, ambao inahofia unaweza kusababisha wimbi jipya la wakimbizi nchini Uturuki.

    Uturuki pia inahisi Brussels inaweza imegeuka makubaliano ya mwaka 2016 na inataka uhakika wa Umoja wa Ulaya kuendelea kufadhili mahitahi ya wakimbizi nchini humo. Chini ya makubaliano ya mwaka 2016 kati ya Ubelgiji na Uturuki, Umoja wa Ulaya ulikubali kuilipa Uturuki Euro bilioni 6 na mambo mengine, ikiweno kuongeza kasi ya kuondoa vizuizi vya visa ili kudhibiti idadi ya wahamiaji wanaelekea Ulaya kupitia Uturuki.

    Tatizo katika Umoja wa Ulaya ni mgawanyo wa ndani kuhusu jinsi ya kugawana mzigo wa kuhudumia wakimbizi na wahamiaji wanaowasili kwenye kundi hilo lenye nchi 21, ingawa maofisa wa Umoja wa Ulaya waliahidi fedha zaidi kwa Ugiriki kukabiliana na mgogoro, wakati wa ziara iliyofanyika jana katika mpaka wa Uturuki na Ugiriki ambao wakimbizi wengi walikuwa wanajaribu kuvuka.

    Mwanadiplomasia mmoja wa Umoja wa Ulaya amesema, Umoja huo umepoteza muda tangu makubaliano ya mwaka 2016, na kufunika tatizo hilo kwa kutoa fedha ili maelfu ya wahamiaji na wakimbizi wabakie nchini Uturuki. Wawakilishi kutoka Netherlands, Italia, Ufaransa na Ujerumani walikuwa kati ya wale waliopendekeza kutoa fedha zaidi kuwasaidia wakimbizi nchini Uturuki, wakitumaini kumfurahisha rais Erdogan.

    Umoja wa Ulaya bado haujajadili kiasi cha fedha zaidi za ufadhili, na wanadiplomasia wanasema uamuzi wowote wa kuongeza fedha unaweza kujadiliwa na viongozi wa nchi wanachama wa Umoja huo, ambao wanatarajiwa kukutana mjini Brussels mwishoni mwa mwezi huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako