• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Maelfu ya watu wanaojitolea wafanya kazi katika mapambano dhidi ya virusi vya Korona

  (GMT+08:00) 2020-03-04 18:25:16

  Wakati madaktari wanajitahidi kuokoa wagonjwa wanaoambukizwa COVID-19, watu wa sekta mbalimbali pia wanasaidia katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo mjini Wuhan. Kuanzia misaada ya matibabu, chakula na bidhaa, na msaada wa kisaikolojia, usafirishaji na huduma za kijamii, maelfu ya watu wanaojitolea wanajibu kwa haraka na kwa makini baada ya Wuhan kufungwa ili kupunguza kuenea kwa virusi hiyo.

  Tarehe 3, Februari, Chama cha Vijana cha Kikomunisti cha China kilitoa taarifa ya kwanza ya kuandikisha watu wanaojitolea, na watu zaidi 7000 walijisajili ndani ya saa 12 baada ya tangazo hilo kutolewa..

  Mpaka sasa, chama hicho kimechagua na kutoa mafunzo kwa watu 19,155 kutoa huduma wakiwa wasambazaji vifurushi, madereva, waratibu na wafanyakazi wa kijamii katika maduka ya bidhaa, vitongoji, hospitali maalum na hospitali za muda za kupokea wagonjwa.

  Tarehe 23, Februari, watu elfu 10 walijisajili upya baada ya kutolewa taarifa mpya za kuandikisha watu wanaojitolea kwa ajili ya kusambaza msaada wa dharura na vifaa vya mahitaji ya maisha kwa wakazi. Yang Xue mwenye umri wa miaka 20, pamoja na rafiki zake wamewapeleka zaidi ya madaktari zaidi ya 800 kwenda kazini na kurudi nyumbani kwa magari. Pia wamesafirisha zaidi ya tani 500 za bidhaa kwa jamii.

  Ili kurahisisha mchakato wa misaada ya nje kupita kwenye forodha, wanafunzi zaidi ya 300 wa vyuo vikuu, wahudumu wa afya na wakalimani walishirikiana kutafsiri nyaraka na taarifa kwa lugha kadhaa za kigeni kama vile Kiingereza, Kijapani, Kikorea, Kirusi, Kijerumani, kifaransa, kiitalia na Kivietnam.

  Mhandisi wa Pakistan anayefanya kazi mjini Wuhan Bw. Haroon Nomaan pia alijitolea kusaidia kuratibu miradi ya nchi za nje na kutafsiri nyaraka 83 za forodha za Kiingereza na Kiurdu.

  Katika miongo kadhaa iliyopita, idadi ya watu wanaojitolea nchini China imeongezeka baada ya maendeleo ya kasi ya uchumi na jamii. Takwimu zinaonyesha kuwa, mjini Wuhan, watu milioni 1.5 wamejisajili kutoa huduma za kujitolea, ambayo ni asilimia 14 ya watu mjini humo.

  Idadi kubwa ya wafanyakazi wa kijamii wenye utaalam pia wamechukua hatua haraka kusaidia watu wenye mahitaji kutokana na maambukizi ya virusi hivyo. Wanachukua hatua za taratibu kusaidia watu kupata huduma, kutoa ushauri na matibabu ya kisaikolojia kwa watu na familia, na kusaidia jamii kutoa na kuboresha huduma za afya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako