• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kizazi kipya cha nzige kitavamia Kenya – FAO

    (GMT+08:00) 2020-03-04 19:06:29

    Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) linalosimamiwa na Umoja wa Mataifa, limeonya kwamba nchi itashuhudia shamblio la kizazi kipya cha nzige wakati wakulima wanapojiandaa kwa msimu wa upanzi.

    Nzige wamevamia zaidi ya kaunti 20 kufikia sasa na kusababisha uharibifu mkubwa kwa mimea ya kilimo na lishe ya mifugo.

    Katika taarifa iliyotolewa Jumatatu, FAO ilisema kuna wasiwasi kuhusu jinsi nzige walioanguliwa majuzi wameanza kukomaa na kujikusanya katika makundi mapya.

    Hali hiyo inaleta hofu ya uhaba wa chakula ambayo inaweza kuhatarisha hali ya maisha ya wananchi siku zijazo.

    Kando na wale wanaoanguliwa Kenya , inahofiwa kuna makundi mapya yanayoweza kushambulia nchi kutoka Somalia kwani wameonekana katika maeneo ya Barbera na Burao yaliyo kaskazini nchini humo.

    Imetabiriwa Kaunti za Marsabit na Turkana ndizo zitakuwa na idadi kubwa zaidi ya wadudu hao waharibifu.

    Mapema wiki hii, waziri wa Kilimo, Bw Peter Munya alisema mpango wa serikali wa kupambana na nzige unaendelea vyema.

    Hata hivyo, alikiri kuna changamoto kukabiliana na shambulio jipya hasa kuhusiana na wadudu watakaotoka Somalia kwani hakuna juhudi zinazoendelezwa kuwaangamiza katika nchi hiyo kwa sababu ya vita vilivyopo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako