• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani yalaumiwa kwa kushambulia tovuti za China

    (GMT+08:00) 2020-03-04 19:23:13

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Zhao Lijian amesema, Marekani inafanya mashambulizi zaidi katika mtandao wa Internet, huku ikizilalamikia nchi nyingine kuifanyia mashambulizi hayo.

    Kampuni ya mtandao wa Internet ya China Qihoo 360 imegundua kuwa, kundi la utapeli linaloshukiwa kuwa la CIA (APT-C-39) limeshambulia mitandao ya internet ya China kwa miaka 11, na kudukua tovuti za mashirika ya anga, mafuta, teknolojia za Internet, na mitandao ya serikali ya China.

    Zhao amesema, China imeathiriwa vibaya na mashambulizi ya Marekani kwenye mtandao wa Internet, na inaitaka Marekani iache mashambulizi hayo, na kuipa dunia mtandao wenye amani, usalama, ushirikiano na wa wazi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako