• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaihimiza Marekani isitishe mashambulizi dhidi ya mtandao wa Internet nchini China

    (GMT+08:00) 2020-03-05 09:43:10

    Kufuatia ripoti iliyotolewa na kampuni ya Qihoo 360 kuhusu mashambulizi yanayofanywa na Marekani dhidi ya mtandao wa Internet nchini China, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Zhao Lijian jana amesema, China inaihimiza Marekani itoe maelezo na kusitisha kitendo hicho mara moja.

    Bw. Zhao amesema ripoti ya kampuni ya Qihoo 360 ni ushahidi muhimu, unaonesha kuwa Marekani ni mshambuliaji mkubwa zaidi wa mtandao wa internetr duniani.

    Kampuni ya mtandao wa Internet ya China Qihoo 360 hivi karibuni imegundua kuwa, kundi la utapeli linaloshukiwa kuwa la Shirika la ujasusi la Marekani CIA (APT-C-39) limeshambulia mitandao ya internet ya China kwa miaka 11, na kudukua tovuti za mashirika ya anga, mafuta, teknolojia za Internet nchini China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako