• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TANZIA:Mchezaji wa raga wa Kenya Simbas na klabu ya KCB Tony Onyango afariki dunia

    (GMT+08:00) 2020-03-05 10:23:22

    Mchezaji wa raga wa Kenya Simbas na klabu ya KCB Tony Onyango amefariki dunia. Onyango alidondoka na kufariki nyumbani kwake Ngong Jumanne usiku akiwa na umri wa miaka 28. Jioni ya Jumatatu alifanya mazoezi na klabu yake huko Ruaraka. Meneja wa klabu ya raga ya KCB Philip Wamae amethibitisha kifo cha mchezaji huyo. Onyango, ameichezea Kenya katika ngazi zote kuanzia chini ya miaka 19 mwaka 2010 hadi timu ya taifa ya Kenya Simbas mwaka 2012 baada ya kupelekwa kwenye timu na Michael "Tank" Otieno na kucheza mechi yake ya kwanza ya majaribio dhidi ya Namibia June 28, 2014. Onyango alikuwa kipenzi cha kocha wa zamani wa Kenya Simbas Jerome Paarwater na mwisho kuicheza Simbas ilikuwa ni dhidi ya Ujerumani Novemba 23, 2018 huko Marseille, Ufaransa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako