• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vijana wa Wuhan wachangia kazi ya kukabiliana na maambukizi

    (GMT+08:00) 2020-03-05 17:57:08

    Leo tarehe 5 Machi ni siku ya vijana wanaojitolea nchini China. Katika mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya korona, mbali na madaktari na wauguzi, vijana wa Wuhan, mji ulioathiriwa vibaya na maambukizi hayo, pia wamejitolea kuchangia katika mapambano hayo.

    Hapo jana idadi ya jumla ya wagonjwa waliopona kwa mara ya kwanza ilizidi ile ya wagonjwa waliothibitishwa kuambukizwa virusi vya korona, na wagojwa wengi wameruhusiwa kuondoka hospitali. Kwa mujibu wa utaratibu, wagonjwa hao wanapaswa kukaa katika nyumba zilizoandaliwa na serikali na kuwekwa karatini kwa siku 14 kabla ya kurudi nyumbani. Hivyo kuwasafirisha wagonjwa ndiyo ni suala jipya, na watu wengi wamejitolea kufanya kazi hii.

    Jana, saa 5 asubuhi, vijana wawili Wang Bo na Yu Liang walifika katika kituo ambacho watu waliojitolea wanakusanyika katika mtaa wa Jiang'an, mjini Wuhan, na kuanza kufanya maandalizi kwa ajili ya kazi.

    Yu Liang mwenye umri wa miaka 24 ni msanifu wa mapambo ya nyumbani. Baada ya mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya korona kuanza, alifikiria angefanya kitu kutoa mchango wake katika mapambano hayo.

    "Mimi ni mwenyeji wa Wuhan. Napenda kuona uhai unarejeshwa katika mji wangu, nataka kufanya kitu. Nilikuwa tayari toka awali, lakini familia yangu hawakukubali. Nikawashawishi, hatua kwa hatua wakakubali. Mwanzoni nilifanya kazi katika hospitali ya muda, kazi kama vile kukusanya vifaa au kusafirisha vitu. Halafu nilipewa kazi ya kuwasafirisha wagonjwa waliopona. Sisi ni kama familia kubwa."

    Baada ya chakula cha mchana, Yu Ling alikwenda nyumba za muda kufanya maandalizi, na Wang Bo alibaki na kusubiri kazi atakayopewa. Saa 7 na nusu, kazi ikaja, alipanda mabasi yaliyoandaliwa kwenda hospitali ya muda ya Jiangxia kuchukua wagonjwa waliopona. Kazi ya Wang Bo ilikuwa kuwasiliana na wafanyakazi wa hospitali, kuhesabu wagonjwa wanaoondoka, na kuhakikisha wanapanda mabasi.

    "Mratibu yuko nyuma. Nilimwambia bado watatu hawajafika, amepiga simu kuwaharakisha. Hii inakwenda vizuri leo. Wagonjwa wanatoka kwa foleni. Kama kuna wagonjwa hawajafika, ni lazima tujue sababu zao na kutoa ripoti. Leo nawapokea watu 40 hivi, wanafanya haraka."

    Mabasi yalifunga safari kuelekea nyumba zilizoandaliwa na serikali, ambapo Yu Liang alikuwa akiwasuburi wagonjwa.

    "Natakiwa kuwakabidhi kwa viongozi wa hapa. Na nilitangulia kuja kujionea hali ya nyumba hizo, mablanketi, mahitaji ya kila siku, usafi wa nyumba, natakiwa kugagua kwanza kila kitu."

    Wagonjwa tayari walijiandikisha kwenye nyumba hizo, vijana hao walirudi kituo cha watu waliojitolea wakisubiri kazi mpya. Kuna siku ambazo wanafanya kazi mpaka usiku wa manane. Wang Bo alisema,

    "Wuhan iko katika kiini cha maambukizi nchini China. Madaktari na wauguzi wengi kutoka sehemu mbalimbali nchini wamekuja Wuhan, pia vifaa na bidhaa zinaendelea kupelekwa. Sisi wenyeji hatuwezi kukaa nyumbani tu, lazima tufanye kitu kuchangia mapambano hayo dhidi ya virusi vya korona."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako