• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania-Serikali yakaza kamba vibali vya mchele

    (GMT+08:00) 2020-03-05 20:13:11
    Serikali ya Tanzania imesema itaendelea kuzuia vibali vya kuagiza nje ya nchi mazao ya chakula yanayozalishwa kwa wingi nchini humo ikiwamo mchele.

    Haya yalisema na Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe katika mkutano wa Baraza la Mchele Tanzania ambao ulikuwa ukijadili uzalishaji bora na endelevu ili kuongeza tija kwa wakulima wa zao hilo.

    Alisema msimamo wa serikali ni kuwa haiwezi kuruhusu uagizaji wa mazao ya chakula ambayo yanazalishwa nchini kwa wingi.

    Alisema kwa sasa Tanzania inazalisha tani milioni 1 za mpunga nan i lazima nchi ijiwekee malengo ili kuwa na uzalishaji wa tani milioni tatu hadi nne.

    Bashe alisema lengo ni kukidhi mahitaji ya nchi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako