• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa UN atoa wito kusitisha mapigano mara moja kati ya Russia na Uturuki nchini Syria

    (GMT+08:00) 2020-03-06 09:51:13

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ameelezea matumaini yake kuwa makubaliano ya hivi karibuni ya kusitisha mapigano kati ya Russia na Uturuki, yatakomesha mapigano katika mkoa wa Idlib nchini Syria haraka na kwa kudumu.

    Rais Vladimir Putin wa Russia na mwenzake wa Uturuki Bw. Recep Tayyip Erdogan wamekubaliana kukomesha mapigano na kuanzisha eneo salama na doria za pamoja.

    Bw. Grterres ametoa wito kurudisha mchakato wa kisiasa uliohimizwa na azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa la mwaka 2015.

    Kwa mujibu wa Ofisi ya uratibu wa masuala ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa, OCHA, Wasyria milioni tano wamekimbia nchi hiyo, wengine milioni sita wamekuwa wakimbizi wa ndani, na wengine zaidi ya watu milioni 13 wanahitaji msaada.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako