• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zimbabwe yajifunza uzoefu wa China katika kukabiliana na COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-07 18:22:24

    Wakati dunia inakabiliwa na maambukizi ya ugonjwa wa nimonia inayosababishwa na virusi vipya vya korona COVID-19, uzoefu wa China wa kukinga na kutibu ugonjwa huo umekuwa msaada mkubwa. Waziri wa afya na ustawi wa watoto wa Zimbabwe Bw. Obediah Moyo amesema, nchi hiyo inaiga uzoefu wa China, ili kuzuia ugonjwa wa COVID-19 usienee nchini Zimbabwe.

    Ikiwa mwenzi wa ushirikiano wa China kwa pande zote, Zimbabwe imedumisha mawasiliano ya karibu ya watu na China. Kutokana na hatua madhubuti zilizochukuliwa na nchi hizo mbili, hadi sasa hakuna maambukizi ya COVID-19 nchini Zimbabwe. Bw. Moyo amesema, kufuatia kuenea kwa ugonjwa huo duniani, Zimbabwe itachukua tahadhari zaidi, na kuongeza uchunguzi kwa watu wanaoingia nchini humo, na pia itaiga uzoefu mzuri wa China katika kukabiliana na ugonjwa huo. Anasema,

    "Uzoefu wa China umethibitisha kuwa nchi hiyo ina uwezo wa kupunguza zaidi maambukizi ya ugonjwa huo. Hivi sasa idadi ya maambukizi na vifo ni chache sana, kutokana na matibabu mwafaka na hatua zenye ufanisi zilizochukuliwa na China. Uzoefu wa China utasaidia sana juhudi za kimataifa katika kukabiliana na maambukizi ya virusi."

    Hivi sasa Zimbabwe imeichukulia Hospitali ya Wilkins kama ni kituo cha karantini na tiba kwa wagonjwa wa COVID-19. Shirika la Afya Duniani WHO limechangia vifaa vya matibabu kwa hospitali hiyo. Mjumbe wa shirika hilo nchini Zimbabwe Dr. Alex Gasasira, amesema China imepata mafanikio mengi katika utafiti wa kisayansi kuhusu ugonjwa wa COVID-19, na mafanikio hayo yatasaidia nchi nyingine kukinga ugonjwa huo na kutibu wagonjwa, kwani dunia inapaswa kushikamana ili kushinda vita dhidi ya ugonjwa huo. Anasema,

    "Virusi vipya vya korona ni virusi visivyojulikana vizuri kwa binadamu. China ina wagonjwa wengi, hivyo imepata uzoefu mkubwa na elimu nyingi. Wakati huo huo nchi nyingine hazina maarifa ya kukabiliana na ugonjwa huo. Wanasayansi wa China wamefanya utafiti kwa wingi, na tunafurahi kuwa wanapenda kutoa uzoefu wao kwa nchi nyingine, zikiwemo nchi za Afrika."

      

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako