• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya wagonjwa wanaoambukizwa COVID-19 yazidi laki 1 duniani

    (GMT+08:00) 2020-03-08 17:41:22

    Shirika la Afya Duniani WHO jana lilitoa taarifa likisema idadi ya wagonjwa walioambukizwa ugonjwa wa nimonia inayosababishwa na virusi vipya vya korona COVID-19 duniani imezidi laki 1, na nchi zote zinapaswa kuchukua hatua madhubuti ili kupunguza maambukizi ya ugonjwa huo.

    Taarifa inasema, uzoefu wa China na nchi nyingine umethibitisha kuwa kuchukua hatua mwafaka kunaweza kupunguza maambukizi hayo na athari yake. Hatua hizo ni pamoja na kujumuisha jamii zote, kuthibitisha wanaoambukizwa, kutunza wagonjwa, kutafuta watu waliokuwa karibu na wagonjwa, kuzifanya hospitali na kliniki zijiandae kukabiliana na ongezeko la wagonjwa, na kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa matibabu.

    Taarifa hiyo pia inasema, WHO itaendelea kushirikiana na nchi zote, wenzi wa ushirikiano na mtandao wa wataalamu, kuratibu majibu ya kimataifa, kutunga sera, kugawanya vifaa, kunufaisha ujuzi, na kutoa habari za kujikinga kwa watu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako