• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ripoti ya UNCTAD yaonyesha mlipuko wa COVID-19 hautapunguza mvuto wa China kwa uwekezaji

    (GMT+08:00) 2020-03-09 09:14:19

    Ripoti ya utafiti iliyotolewa na Kamati ya Umoja wa Mataifa ya biashara na maendeleo, UNCTAD imesema mlipuko wa virusi vipya vya korona duniani unakadiriwa kupunguza uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nchi za nje kwa asilimia 5 hadi asilimia 15 mwaka huu.

    Mkuu wa idara ya uwekezaji na biashara wa UNCTAD Bi. Zhan Xiaoning amesema ingawa China itaathiriwa na mazingira ya jumla ya uwekezaji duniani, janga hilo halitapunguza mvuto wa China kwa uwekezaji kutoka nje.

    Bibi Zhan ameongeza kuwa China imeendelea kufungua mlango, na kuchukua hatua mbalimbali mpya, ikiwa ni pamoja na kufanyia uvumbuzi mfumo wa mitaji ya kigeni na kazi ya kuvutia uwekezaji kutoka nje, hivyo kwa kasi kubwa au ndogo, uchumi wa China utaendelea kukua.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako