• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • COVID-19 yasababisha upungufu wa uwekezaji wa moja kwa moja duniani

    (GMT+08:00) 2020-03-09 17:25:12

    Ripoti iliyotolewa katika mkutano wa biashara na maendeleo wa Umoja wa Mataifa UNCTAD imeonyesha kuwa, kutokana na maambukizi ya COVID-19, uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje duniani katika mwaka 2020 unatarajiwa kupunguza kwa asilimia 5 hadi asilimia 15. Hata hivyo, ingawa China pia itaathiriwa na mazingira ya jumla ya uwekezaji duniani, maambukizi hayo hayatabadili hali ya kimsingi ya China kuvutia uwekezaji kutoka nje.

    Ripoti ya UNCTAD imeonyesha kuwa, maambukizi ya COVID-19 huenda yatafanya uwekezaji wa moja kwa moja kufikia kiwango cha chini zaidi tangu mwaka 2008. Mkuu wa idara ya uwekezaji na viwanda ya UNCTAD Bw. Zhan Xiaoning amesema, "Kutokana na tathimini ya awali, uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje duniani huenda utapungua kwa asilimia 5 hadi asilimia 15. Hiyo inategemea maendeleo ya maambukizi ya COVID-19, kama maambukizi hayo yatamalizika kote duniani katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, upungufu huo utafikia asilimia 5 hivi, kama yataendelea mpaka mwishoni mwa mwaka huu, yataathiri uwekezaji huo mwaka mzima, na upungufu utafikia asilimia 15."

    Bw. Zhan amesema, ingawa China pia itaathiriwa kutokana na mazingira ya jumla ya uwekezaji duniani, lakini maambukizi hayo hayatabadilisha hali ya kimsingi ya China kuvutia uwekezaji kutoka nje. Amesema, uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje unaamuliwa na vyanzo vitatu, sera, msingi wa uchumi na urahisi wa uwekezaji. Bw. Zhan amesema nguvu za China za kufungua mlango zitaendelea kuongezeka.  Anasema, "China itaendelea kuongeza nguvu za kufungua mlango, kuendelea kuchukua hatua mbalimbali mpya, zikiwemo uvumbuzi wa mfumo wa mitaji kutoka nje, na uvumbuzi wa kuvutia wafanyabiashara na uwekezaji. Sera zetu ni nzuri kuliko nchi nyingine nyingi, hasa zile zinazoshindana na China katika kuvutia uwekezaji. Kwa mfano, nchi zilizoendelea zimeonesha hali ya kujilinda kibiashara, lakini China inaendelea kufungua mlango zaidi kwa nje. "

    Bw. Zhan amesema, uchumi wa China ni mkubwa, bila kujali kasi ya ongezeko ni kubwa au ndogo, ukubwa wa jumla unaongezeka siku hadi siku, mapato ya wastani ya kila mtu yanaongezeka, na huo ndio mwekeleo unaoshuhudiwa. Katika hali ya kurahisisha uwekezaji, miundo mbinu ya China na sifa ya nguvukazi zinaboreshwa siku hadi siku.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako