• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UM waihimiza Sudan Kusini kuharakisha utekelezaji wa mpango wa usalama

    (GMT+08:00) 2020-03-10 08:47:18

    Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS imewahimiza rais Salva Kiir na makamu wake wa kwanza Riek Machar kuharakikisha utekelezaji wa makubaliano ya mpango wa usalama ili kuimarisha mchakato wa amani nchini humo.

    Kiongozi wa UNMISS na mjumbe maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini Bw. David Shearer, amesisistiza haja ya dharura ya kutekeleza mpango wa usalama baada ya kuvunjwa kwa Kamati ya Taifa ya Kabla ya Mpito NPTC, wakati pande hasimu nchini humo zinasubiri kuunda baraza la serikali ya umoja ya mpito.

    Bw. Shearer amelaani kupamba moto kwa mgogoro wa kikabila katika majimbo ya Jonglei na Pibor kutokana na kuchelewa kwa uteuzi wa viongozi wa serikali ya huko, ambao umesababisha vifo vya watu wengi na maelfu ya familia kukimbia makazi yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako