• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WHO yasema maambukizi ya COVID-19 yameenea duniani

    (GMT+08:00) 2020-03-10 09:11:30

    Mkurugenzi wa Shirika la afya duniani WHO Bw. Tedros Ghebreyesus amesema, maambukizi ya nimonia inayosababishwa na virusi vipya vya korona COVID-19 yametokea katika nchi nyingi duniani, na tishio la kuenea kwa maambukizi ya ugonjwa huo duniani limekuwa halisi.

    Lakini Bw. Ghebreyesus amesisitiza kuwa, licha ya changamoto kubwa, maambukizi ya COVID-19 litakuwa janga la kwanza la maambukizi ya ugonjwa litakaloweza kudhibitiwa katika historia.

    Amesema kutokana na kuongezeka kwa idadi ya wagonjwa na nchi na sehemu zinazoathiriwa na ugonjwa huo duniani, nchi mbalimbali zinatakiwa kuchukua hatua zenye ufanisi, kukinga na kuzuia ugonjwa huo kwa wakati mmoja.

    Vilevile anazitaka nchi zote kufuata mkakati shirikishi ili kudhibiti maambukizi ya ugonjwa huo, na kwamba nchi zile zinazogundua maambukizi, na kuwafuatilia watu waliokaribiana na walioambukizwa, si kama tu zinawalinda watu wa nchi zao, bali pia hatua hizo zitasaidia kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo katika nchi nyingine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako