• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa Italia atangaza kufunga miji kote nchini ili kuzuia kuenea kwa maambukizi ya COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-10 09:11:44

    Waziri mkuu wa Italia Bw. Giuseppe Conte, amesema ili kuzuia kuenea kwa maambukizi ya nimonia inayosababishwa na virusi vipya vya korona COVID-19, Italia itatekeleza hatua za kufunga miji kote nchini kuanzia leo. Amesema mbali na sababu tatu maalumu za kazi, afya na mahitaji ya dharura zinazothibitishika, wananchi wote hawatakiwi kuondoka kutoka sehemu wanazokaa.

    Hatua hizo pia ni pamoja na kuanzia leo mashindano yote ya michezo nchini humo yakiwemo Ligi kuu ya Italia yatasimamishwa, na kurefusha muda wa kufungwa kwa shule kuanzia tarehe 15 Machi hadi tarehe 3 Aprili.

    Serikali ya Italia pia imethibitisha kuwa, Idadi ya watu walioambukizwa COVID-19 imefikia 7,985, na idadi ya vifo imefikia 463.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako