• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Gor Mahia washinda mechi yao dhidi ya AFC Leopards

    (GMT+08:00) 2020-03-10 16:36:21

    Timu ya Gor Mahia maarufu K'Ogalo imeendeleza ubabe dhidi ya wapinzani wako wakubwa AFC Leopards ama Ingwe kwa kuibuka na ushindi wa bao 1 – 0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Kenya uliochezwa jumapili kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Moi Kasarani. Bao pekee la Gor Mahia lilifungwa na Boniface Omondi katika dakika ya 27. Ushindi huo umeifanya K'Ogalo kuifunga Ingwe mara mbili, ambapo katika mchezo wa kwanza walishinda kwa bao 4 – 1. Mpaka sasa, Gor Mahia wanaongoza Ligi hiyo kwa kuwa na point 54 huku AFC Leopards wakiwa nafasi ya sita kwa pointi 40.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako