• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China kuchukua hatua mbalimbali kuhakikisha kuondoa umaskini kwa sifa ya juu

  (GMT+08:00) 2020-03-10 18:55:46

  China imepanga kukamilisha kazi ya kuondoa umasikini katika maeneo ya vijijini mwaka huu wa 2020, na hiyo ni ahadi iliyotolewa na Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, ambayo ni lazima itimizwe kwa wakati uliopangwa. Katika semina ya kuondoa umaskini, rais Xi Jinping wa China ametoa amri mpya ya kupata ushindi katika mapambano dhidi ya umaskini.

  Katika kijiji cha Shangjiang, wilaya ya Longzhou, mjini Chongzuo, mkoani Guangxi, wafanyakazi wa kuwasaidia watu maskini na wakazi wanashirikiana kulima shamba la matunda ya passion. Rais Xi amesema ni lazima kuchukua hatua mbalimbali kuimarisha mafanikio ya kuondoa umaskini, kuongeza nguvu za kuwasaidia watu maskini, na kuzingatia maendeleo ya sekta za kilimo. Mfanyakazi wa kuwasaidia watu maskini katika kijiji cha Shangjiang Bw. Liang Jingjian amesema, kauli ya rais Xi imetoa mwelekeo na kuimarisha imani ya kuendeleza kilimo maalumu, na kutimiza lengo la kuondoa umaskini na kuongeza kipato. Amesema,

  "Tutaendelea kuendeleza sekta ya kilimo ya anise na matunda ya passion, kuwaongoza watu wote kijijini kutajirika kwa pamoja bila kusahau yeyote. "

  Katika mkoa wa Guizhou, miji mbalimbali inatoa kipaumbele kutatua tatizo la nguvukazi kutoka sehemu zilizoko nyuma kimaendeleo kupata ajira, kubadilisha muundo wa uchumi, na kuimarisha sekta ya kilimo, ili kuhakikisha wakazi wanaongeza mapato. Kiwanda kimoja cha miwani katika eneo la kuendeleza uchumi la mji wa Tongren kimerejesha uzalishaji tarehe 17 Feburari, mpaka sasa wafanyakazi zaidi 40 wamerejea kazini na kuzalisha maelfu ya miwani kila siku. Meneja wa kiwanda hicho Bw. Yang Zhengguo amesema,

  "Katika kipindi hiki cha kurejesha uzalishaji, makada wa eneo hili wanakuja mara kwa mara kueleza kazi ya kinga na tiba maambukizi ya COVID-19, pia kuratibu vifaa vya matibabu, na kutatua masuala tunayokabiliwa nayo. "

  Takwimu zinaonyesha kuwa, mpaka sasa wilaya 52 nchini China bado ziko kwenye umaskini, na watu waliosajiliwa katika vijiji 2,707 bado wako hali ya umaskini. Ingawa idadi hiyo si kubwa, lakini wako katika umasikini uliokithiri. Rais Xi kwenye semina ya kuondoa umaskini amesema, serikali kuu inapaswa kuongeza fedha za kuwasaidia watu maskini, serikali za ngazi mbalimbali pia zinapaswa kuhakikisha kukidhi mahitaji ya kifedha ya kuondoa umaskini. Pia amesema inapaswa kuzidisha ushirikiano kati ya sehemu za mashariki na magharibi, na msaada wa kuondoa umaskini unaotolewa na idara za serikali kuu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako