• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa wawataka viongozi wa Puntland kuwa na umoja na maafikiano ili kuondoa mvutano

    (GMT+08:00) 2020-03-10 19:02:25

    Mjumbe wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, James Swan, amewataka viongozi katika eneo la Puntland nchini humo kuwa na umoja na maafikiano na serikali kuu ya Somalia ili kusaidia kuondoa mvutano kati ya pande hizo mbili kuhusu njia sahihi ya kuendelea mbele.

    Bw. Swan amesema hayo baada ya kufanya mkutano na rais wa Puntland Said Deni mjini Garowe, na kuongeza kuwa viongozi wa Somalia wanapaswa kuungana pamoja kukabiliana na changamoto zinazoikabili nchi hiyo.

    Amesema maendeleo na changamoto ambazo bado hazijatatuliwa kuhusiana na kipaumbele cha kitaifa cha Somalia kwa mwaka huu, ikiwemo kufanya uchaguzi wa mtu mmoja, kura moja, kuimarisha usalama na kutimiza katiba ya nchi, ni kati ya ajenda zilizozungumzwa katika mkutano wake na rais Deni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako