• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Floyd Mayweather ataka kuinunua Newcastle United

    (GMT+08:00) 2020-03-11 12:01:23

    Mwanamasumbwi machachari raia wa Marekani, Floyd Mayweather a.k.a 'Money' ameonesha nia yake ya kutaka kuinunua klabu ya Newcastle United inayoshiriki Premier League. Bingwa huyo wa dunia, 'Money' ameongea hayo wikiend iliyopita akiwa kwenye sherehe nyakati za jioni kwenye 'tour' yake huko 02 City Hall. Mashabiki wa Newcastle United wamekuwa wakimtaka mmiliki wa klabu hiyo ya England, Bilionea Mike Ashley kuiuza baada ya uongozi wake wa miaka 13 pasipo mafanikio yoyote. 'Money' ni bondia mwenye mafanikio makubwa ndani na nje ya uwanja, anaaminika kuwa miongoni mwa wanamichezo wanao miliki mkwanja mrefu zaidi. Mmarekani huyo mwenye umri wa miaka 43, katika mapambano 50 aliyopigana ameshinda yote, hajapoteza hata moja. Ikumbukwe aliwahi kupigana na nyota wa UFC, Conor McGregor, amewahi pia kupambana na Oscar De La Hoya, Ricky Hatton, Manny Pacquiao na Canelo Alvarez ndani ya miaka yake 20 ya tasnia hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako