• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Tanzania yaichapa Liberia U16

    (GMT+08:00) 2020-03-11 16:53:56

    Timu ya Taifa ya Tanzania chini ya miaka 16 imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Liberia katika mashindano maalum yanayofanyika nchini Tanzania. Mchezo huo ni wa kwanza kufuatana na ratiba ya michuano hiyo inayofanyika nchini humo kwa timu za vijana walio chini ya miaka 16. Mashindano hayo yanajumuisha washiriki watatu ambao ni Tanzania (mwenyeji), Liberia na Malawi. Timu ya vijana chini ya umri wa miaka 16 inaandaliwa kwa ajili ya kushiriki fainali za Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17, zitakazofanyika mwaka 2021, nchini Morocco.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako