• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China aapa ushindi wa vita dhidi ya COVID-19 katika mstari wa mbele

    (GMT+08:00) 2020-03-11 17:35:42

    Jana jumanne, rais Xi Jinping wa China alikwenda mjini Wuhan ambao ni mstari wa mbele zaidi wa mapambano dhidi ya COVID-19, na kutoa amri ya kupata ushindi dhidi ya virusi hiyo. Hii ni mara nyingine ya rais Xi kukagua kazi ya kinga na udhibiti wa maambukizi ya virusi hivyo baada ya kukagua mara mbili kazi hiyo mjini Beijing. Lakini safari hii amekwenda kwenye mji ambao ni kiini cha maambukizi ya virusi hiyo nchini China. Watu wanaona ziara hiyo ina maana kubwa.

    Wakati rais Xi akifanya ziara hiyo mjini Wuhan, tayari hospitali 14 za muda zilizoanzishwa kwa ajili ya matibabu ya wagonjwa wa COVID-19 zimefungwa, jambo linalowafanya wataalamu kuona kuwa, vita dhidi ya COVID-19 nchini China inakaribia kumalizika.

    Ndani ya miezi miwili, China imegeuza hali ya maambukizi hayo, na jamii ya kimataifa inaamini kuwa, hatua hiyo imefikiwa kutokana na ushirikiano na juhudi kubwa za pamoja kati ya uongozi imara wa serikali ya China na wananchi wake.

    Rais Xi amekuwa mstari wa mbele katika kuongoza kazi ya kukinga na kudhibiti ugonjwa huo, kuendesha mikutano 6 ya kamati ya kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Chama cha Kikomunisti cha China ndani ya siku 40, kufanya ukaguzi mara tatu, na kutumia vitendo halisi kueleza wazo la utekelezaji wa siasa ya Chama cha Kikomunisti cha China, ambalo ni "kufuatilia watu".

    Kwa sasa, maambukizi ya COVID-19 yameenea kote duniani, Shirika la Afya Duniani WHO limeeleza wasiwasi juu ya baadhi ya nchi kutotilia maanani na kutojiandaa vizuri. Hadi saa 5 usiku wa tarehe 10 kwa saa za Marekani ya mashariki, majimbo 37 ikiwemo Washington zimeripoti kesi za maambukizi ya COVID-19, na idadi ya jumla imezidi elfu moja, huku 31 kati yao wamefariki. Mkuu wa jimbo la New York amesema, serikali ya Marekani imechelewa kuchukua hatua za kukabiliana maambukizi hayo. Nacho kituo cha Habari nchini humo CNN pia kimesema sasa ni wakati mbaya zaidi kwa Wamarekani, na kitendo cha serikali ya Marekani kutochukua hatua za kutosha kimeifanya nchi hiyo kuwa katika hali ya hatari.

    Jumuiya ya kimataifa imeona wazi kuwa, maambukizi ya COVID-19 ni mtihani kwa kila nchi, pia ni fursa kwa dunia nzima kukagua na kutathimini vitendo vya nchi mbalimbali. Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Ghebreyesus amesema, alipokuja Beijing aliona rais Xi alivyoongoza kazi ya kinga na udhibiti wa maambukizi hayo, na WHO inatoa wito wa kuwa na nguvu za uongozi na nia ya kisiasa, vitu ambavyo kiongozi wa China amevionyesha.

    Akiwa mjini Wuhan, rais Xi ametoa amri ya kuendeleza juhudi wakati vita dhidi ya COVID-19 imepata ushindi wa kipindi, na kuonyesha kwa mara nyingine tena imani, nia na uwezo wa China, pia imeonyesha ushindi wa China katika vita hiyo unakaribia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako