• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sekta ya utalii nchini Afrika Kusini yapata hasara kubwa kutokana na mlipuko wa COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-11 17:53:01

    Waziri wa utalii nchini Afrika Kusini Mmamoloko Kubayi-Ngubane amesema, sekta hiyo imepata hasara kubwa kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa nimonia inayosababishwa na virusi vipya vya korona COVID-19, na hatua mpya za kukabiliana na changamoto hiyo zinapaswa kuchukuliwa.

    Akizungumza katika mkutano na wadau wa sekta ya utalii uliofanyika Johannesburg, Bi. Kubayi-Ngubane amesema mlipuko wa virusi hivyo umeathiri sekta hiyo vibaya, kwani mnyororo wa ugavi wa utalii unajumuisha kila kitu kuanzia kilimo, uvuvi na hata sekta ya benki. Ameongeza kuwa, jinsi vizuizi vinavyoendelea, ndivyo athari kubwa itakavyoendelea katika maeneo muhimu ikiwemo hoteli, chakula na huduma ya vinywaji.

    Waziri huyo amesema, wizara yake itashirikiana na wadau hao kutekeleza hatua kadhaa ambazo zitasaidia kupunguza athari hizo kwa wafanyabiashara na wananchi wa kawaida.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako