• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapongeza juhudi za Burundi za kudumisha utulivu wa nchi

    (GMT+08:00) 2020-03-11 17:53:25

    Mjumbe maalum wa masuala ya haki za binadamu katika Wizara ya Mambo ya Nje ya China Liu Hua amesema, China inapongeza juhudi nzuri zinazofanywa na serikali ya Burundi katika miaka ya karibuni kudumisha utulivu wa kitaifa na kuboresha maafikiano ndani ya nchi.

    Akizungumza kwenye mkutano wa Baraza la 43 la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa unaofanyika mjini Geneva, Liu amesema China inapongeza hatua zilizochukuliwa na serikali ya Burundi katika kuboresha uchumi na maendeleo ya jamii, na pia ulinzi wa haki za binadamu. Ameongeza kuwa, China inaamini kuwa jamii ya kimataifa inapaswa kuheshimu serikali na watu wa Burundi, kurejesha na kuongeza ushirikiano wa kiuchumi na misaada ya maendeleo kwa Burundi, na kuchukua nafasi chanya katika mchakato wa maafikiano na maandalizi ya uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Mei nchini humo

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako